Maafisa wa EACC wavamia makazi na afisi za gavana wa Kiambu

  • | KBC Video
    4,141 views

    Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi Jumanne ilitekeleza oparesheni kali iliyolenga makazi na afisi za Gavana wa kaunti ya Kiambu Kimani Wamatangi na maafisa wanane wakuu wa kaunti hiyo. Operesheni hiyo inafuatia madai ya ununuzi usiofuata utaratibu na wa uwongo ambao inasemekana uligharimu wakazi wa kaunti hiyo zaidi ya shilingi bilioni 1.5. Wakati wa oparesheni hiyo, maafisa hao walilazimika kutumia vitoza machozi kutawanya umati uliojaribu kuzuia kukamatwa kwa Gavana huyo. Gavana Wamatangi na maafisa waliohusishwa na kashfa hiyo baadaye walipelekwa katika makao makuu ya tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC katika jumba la Integrity jijini Nairobi kurekodi taarifa na baadaye wakaachiliwa huru wakisubiri kufikishwa mahakamani. Mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim ana maelezo zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News