Maafisa wa polisi waagizwa kukabiliana na 'panga boys' Diani

  • | Citizen TV
    6,537 views

    Kamanda wa polisi eneo la Pwani Ali Nuno amesema maafisa wa polisi watakaozembea kwenye juhudi za kukabiliana na magenge ya vijana wadogo wanaohangaisha kwa mapanga wakaazi wa Diani kaunti ya Kwale wataondolewa. Akizungumza kwenye baraza la umma eneo la Jogoo, kamanda huyo ameamrisha vitengo vya usalama mjini humo kukabiliana na magenge hayo chini ya siku saba.