Maafisa wa polisi wafanikiwa kuwadhibiti waasi wa Oromo Liberation Army mwa Kenya

  • | Citizen TV
    6,692 views

    Kikosi cha pamoja kinachojumuisha maafisa kutoka idara ya polisi kimepiga hatua kubwa katika kuwadhibiti waasi wa Oromo Liberation Army (OLA), ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiwahangaisha wakazi wa Marsabit na Isiolo. Kikosi hicho, kilianza kazi Januari mwaka huu chini ya operesheni ondoa jangili. Tangu kuzinduliwa kwa operesheni hiyo, maficho ya waasi wa OLA katika kaunti hizo mbili yamevurugwa, hatua ambayo imelemaza pakubwa shughuli za kundi hilo. Aidha, wanachama kadhaa, wakiwemo makamanda wa ngazi za juu, wamekamatwa kwenye msako unaoendelea. Ben Kirui amerejea kutoka marsabit na isiolo na kutuandalia taarifa ifuatayo.