Maafisa wa polisi wateka nyara Billy Mwangi mjini Embu

  • | Citizen TV
    8,876 views

    Siku Moja Baada Ya Runinga Ya Citizen Kuangazia Kisa Cha Utekaji Nyara Wa Peter Muteti Katika Eneo La Uthiru Kwa Kuchapisha Picha Iliyomdhalilisha Rais William Ruto, Familia Nyingine Mjini Embu Imejitokeza Na Kudai Kutekwa Nyara Kwa Mwanawao Billy Mwangi Kwa Kosa Sawia La Kuchapisha Taarifa Kwenye Mtandao Wa X Uliokisiwa Kuashiria Mauti Kwa Kiongozi Wa Taifa. Mwangi Alitekwa Nyara Na Watu Wanaoaminika Kuwa Maafisa Wa Usalama Mjini Embu Mwendo Wa Saa Tisa Mchana. Visa Hivyo Viwili Vimezua Tetesi Kutoka Kwa Viongozi Wa Kisiasa Ambao Wametaka Serikali Kuwaachilia Wawili Hao Na Kuwachukulia Hatua Iwapo Wana Makosa