Maafisa wakuu katika ofisi ya Gachagua wafurushwa nje

  • | Citizen TV
    19,775 views

    Maafisa wakuu katika afisi ya naibu Rais aliyeondolewa na seneti Rigathi Gachagua wameamrishwa kwenda likizo ya lazima. Wafanyikazi hao zaidi ya mia moja wametakiwa kuanza likizo mara moja huku serikali ikiendelea na kile ilichotaja kama mchakato wa kikatiba unaoendelea na ambao unaathiri afisi ya Naibu Rais. Na kama anavyotuarifu Brenda Wanga Miongoni mwa waliotimuliwa ni washauri tisa wa Rigathi Gachagua.