Maajabu ambayo hufanya bahari kuwa ya buluu usiku

  • | BBC Swahili
    634 views
    Wakazi wa kusini mwa California nchini Marekani wanamiminika kwenye ufukwe wa bahari kushuhudia tukio la asili linalofanya maji kuwa ya buluu usiku. Hii kwa jina la kitaalamu inaitwa 'bioluminescence' - ambapo ni mwanga unaotolewa na aina mojawapo ya mwani wa baharini unapobugudhiwa. Drew Lucas, mtaalam kutoka Taasisi ya Scripps ya Oceanography, aliiambia CBS News kwamba mwani hustawi katika hali ya joto na hali ya utulivu ambapo kusini mwa California imekuwa ikipata hali hiyo hivi karibuni. #bbcswahili #califonia #mwani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw