Machifu waliotekwa nyara Mandera kurejeshwa nyumbani

  • | KBC Video
    1,187 views

    Machifu watano waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabaab katika kaunti ya Mandera mnamo mwezi Februari wameachiliwa. Machifu hao walitekwa nyara wakati walipokuwa wakisafiri kutoka eneo la Wargadud kuelekea Elwak.Waziri wa usalama wa taifa, Kipchumba Murkomen, ambaye ameanza ziara ya siku sita eneo la Pwani alisema machifu hao sasa wamo mikonono mwa maafisa wa serikali ya Kenya na watawasili humu nchini hivi karibuni. Alisiffia juhudi za pamoja za serikali kuu na zile za kaunti pamoja na ushirikiano wa jamii kwa kufanikisha kuachiliwa kwa machifu hao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive