Machifu waliotekwa nyara Mandera waungana na familia zao

  • | KBC Video
    99 views

    Machifu watatu waliokuwa wametekwa-nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al-shabaab katika kaunti ya Mandera na baadaye kuachiliwa huru, wameungana na familia zao. Machifu hao, ambao ni pamoja na Mohammed Adawa, Mohammed Hassan, Abdi Hassan, Mohmmed Noor Haache pamoja na naibu wa chifu Ibrahim Gabow, walidhihirisha furaha yao baada ya kukutana na wapendwa wao. Machifu hao ambao walikuwa mikononi mwa kundi hilo la wapiganaji kwa muda wa miezi miwili, walisimulia yaliojiri, huku waziri wa usalama wa taifa, Kipchumba Murkomen, akiapa kuhakikisha visa kama hivyo havitashuhudiwa tena.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive

    shabaab