Mafanikio ya mradi ili kuzuia migogoro ya wakulima na wafugaji

  • | VOA Swahili
    50 views
    Ukame, ardhi kugeuka jangwa, ukataji miti na mabadiliko ya hali ya hewa Kaskazini mwa Nigeria yamewalazimisha wafugaji kuhamia kusini wakitafuta maeneo ya malisho kwa mifugo.⁣ ⁣ Harakati hii imepelekea hasara ya zaidi ya maisha elfu 60 kwa mujibu wa spika wa Baraza la Wawakilishi la Nigeria.⁣ ⁣ Kuzungumzia suala hili, mradi wa kilimo na ufugaji ulizinduliwa huko Kano, na kuweka makazi, maeneo ya malisho na vituo vya ukusanyaji maziwa ili kuwazuia wafugaji kupambana na wakulima.⁣ ⁣ Ibrahim Garba Mohammed ni mratibu wa mradi wa kilimo na ufugaji katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano. Mradi unajumuisha maeneo ya malisho na makazi ya wafugaji wa Fulani ambayo yamefadhiliwa na “Lives, livelihood Funds” LLF na ‘Benki ya Maendeleo ya Kiislamu.’ Lengo ni kutokomeza ghasia kote Nigeria.⁣ ⁣ ⁣ Ibrahim Garba Muhammad, Mratibu wa Mradi wa Kilimo na Ufufaji anaeleza: “Kuanzia sasa, tumewapatia chanjo zaidi ya mifugo milioni 3 katika jimbo hili. Kwa kuongezea, tumeweka maabara, ya kwanza ya aina yake kaskazini mwa Nigeria. Pia tumeandikisha wafanyakazi wa kijamii 220 kuangalia mifugo.”⁣ ⁣ Kwa miongo mingi, wakulima na wafugaji wamejihusisha na mzozo. Wakulima wanawashutumu wafugaji kwa kuiba mazao yao, wakati wafugaji walijihusisha na mashambulizi ya kulipiza kisasi wakiwalaumu wakulima kwa kunyakua maeneo ya malisho.⁣ ⁣ Kufanya mambo yawe mabaya zaidi, kuongezeka kwa hali ya ukavu, kaskazini mwa Nigeria, ukame na upanuzi wa ardhi ya kilimo kumepunguza ardhi ya malishi na kuchochea mizozo kwa kiasi fulani ya nchini Nigeria.⁣ ⁣ Mshauri wa kilimo Bello Abba Yakasai anasema kwamba kuhakikisha usalama kwa maeneo la malisho kwa ajili ya wafugaji ni muhimu sana kwa uendelevu wao, hasa katika kupambana na tishio la wizi wa ng’ombe.⁣ ⁣ ⁣ ⁣ ⁣ ⁣#nigeria #mgogoro #ardhi #mifugo #mapigano #vita #serikali ⁣ #voa #voaswahili #suluhisho ⁣ ⁣ Ripoti ya mwandishi wa VOA Alhassan Bala⁣