'Maficho ya jumuiya ya kigaidi ya Hamas yakiangamizwa'

  • | VOA Swahili
    559 views
    Jeshi la Israeli limesema Jumatano wanajeshi wake ambao wamekuwa wakiendesha operesheni za kijeshi katika eneo la Khan Younis kwa siku kadhaa zilizopita wamegundua silaha mbalimbali, nyaraka za kijasusi na mahandaki.⁣ ⁣ Hivi sasa Jeshi hilo linajikita katika operesheni kubwa mbalimbali huko kusini mwa mji wa Khan Younis na kambi za wakimbizi zilizoko katikati ya Gaza ambazo ziko tangu mwaka 1948 zikizunguka mahali Israel ilipoundwa.⁣ ⁣ Mamia ya watu wameuawa katika siku za karibuni kutokana na mashambulizi yanayoendelea katika eneo lote hilo, ikiwemo maeneo ya mbali kusini ambapo watu waliambiwa waende kutafuta hifadhi.⁣ ⁣ Tangu vita ilipoanza, mashambulizi ya Israel yameuwa zaidi ya Wapalestina 23,000, ikikadiriwa ni asilimia 1 ya idadi ya watu katika eneo hilo, na zaidi ya watu 58,000 wamejeruhiwa, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo la Gaza linalosimamiwa na Hamas.⁣ ⁣ Takriban theluthi mbili ya waliofariki ni wanawake na watoto, maafisa wa afya wamesema. Idadi ya vifo haitofautishi kati ya wapiganaji na raia.⁣ ⁣ Katika shambulizi la Oktoba 7, ambapo Hamas walivishitukiza vikosi vya ulinzi mbalimbali vya Israel na kuvamia jamii kadhaa, wanamgambo hao wa Palestina waliwauwa watu 1,200, wengi wao raia.⁣ ⁣ Waliwateka kiasi cha wengine 250, karibu nusu yao waliachiliwa huru katika kipindi cha wiki moja cha kusitishwa mapigano mwezi Novemba.⁣ -AP ⁣⁣ #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi