Mahakama yadinda kusimamisha zoezi la kumuondoa Gachagua

  • | Citizen TV
    8,189 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua amepata pigo baada ya mahakama kuu kukata kulizuia bunge la Seneti kujadili na kuamua hoja ya kumuondoa mamlakani. Jaji Chacha Mwita badala yake akiamua kuwa bunge la seneti lina haki kuendelea na hoja inayoendelea ya kumuondoa mamlakani. Haya yanajiri huku kesi nyingine iliyo mbele ya majaji watatu walioteuliwa na jaji mkuu kusikiza kesi 6 zilizowasilishwa kumtetea Gachagua zikipangiwa kusikilizwa siku ya Jumatano.