Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Matifa UN Jean- Pierre La Croix ametangaza kuwa UN imepewa mamlaka yote kusaidia kifedha kikosi cha SADC kwa ajili ya kudumisha amani na usalama mashariki mwa DRC. Alifahamisha hayo wakati wa ziara yake huko Kivu Kaskazini.
Akizungumuza na waandishi wa habari dakika chache baada ya kukutana na kamati ya usalama wa Mkoa wa Kivu Kaskazini inayosimamiwa na Gavana wa Kivu Kaskazini, Meja Jenerali Peter Cirimwami siku ya Alhamisi, Jean – Pierre la Croix amesema kwa sasa ni muhimu kwa DRC na MONUSCO kushirikiana, kwani Umoja wa Mataifa umepewa mamlaka ya kuwasaidia wanajeshi wa SADC kifedha na huduma nyingine kwa ajili ya kurejesha amani na usalama mashariki mwa Congo.
“Kwa sasa tumepewa mamlaka ya kusaidia SAMIDRC kupitia MONUSCO kupitia njia za kidiplomasia na kisiasa na kuunga mkono juhudi za SADC na kikanda. Tunaunga mkono hata hivyo usitishwaji wa mapigano ambao umepunguza ghasia licha ya kuwepo matatizo madogo , kuna mambo mengi ya kufanya na hatuwezi kusema kwamba pande husika zimeheshimu kikamilifu sitisho la mapigano,” La Croix alisema.
La Croix alitembelea mkoa wa Ituri ambako kumekuwa kukiripotiwa mauaji kila siku na kulazimisha wakazi kuhama vijiji vyao.
Wakimbizi wa ndani katika mkoa huo wanakabiliwa na ukosefu wa misaada
Ripoti/ Picha na Mahojiano na Austere Malivika
21 Apr 2025
- As an at-times unwitting star on social media, Pope Francis knew how to exploit the internet to preach the gospel, broadening the Church's appeal while modernising its communications.
21 Apr 2025
- US Defense Secretary Pete Hegseth fought back Monday -- with White House support -- against another scandal over his reported use of Signal to discuss airstrikes on Yemen, this time with his wife, brother and lawyer.
21 Apr 2025
- President William Ruto will visit Beijing and meet with President Xi Jinping as reciprocal trade tariffs between America and Beijing deepen, and shockwaves in the aftermath of the tariffs rip through the global markets.
21 Apr 2025
- Some cardinals who are being talked about as "papabili" to succeed Pope Francis, whose death at the age of 88 was announced by the Vatican on Monday.