Mahojiano na Dkt. Salome, katibu mkuu wa idara ya kurekebisha tabia- Mwanamke na uongozi

  • | K24 Video
    78 views

    Jamii inahimizwa kuwapa fursa wafungwa waliomaliza vifungo vyao ili waweze kuanza maisha mapya kwa urahisi. Katibu mkuu wa idara ya kurekebisha tabia, dkt. Salome Beacco, ameweka wazi kuwa wafungwa hupitia mchakato wa marekebisho ya tabia, akisisitiza kuwa mtu mwenye makosa anaweza kubadilika kuwa mwema. Magereza 135 nchini yanahudumia wafungwa wapatao 62,000. Katika makala ya “mwanamke na uongozi,” dkt. Salome alielezea pia nafasi yake kama kiongozi katika wizara ya usalama, akiwahimiza wanawake kuchukua nafasi za uongozi katika sekta hiyo.