Majaji wakataa kujiondo kwenye kesi ya kumuondoa naibu rais Rigathi Gachagua ofisini

  • | Citizen TV
    99,766 views

    Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu wanatoa uamuzi kuhusu kujiondoa kwenye kesi ya kutimuliwa kwa rigathi gachagua baada ya baadhi ya mawakili kutilia shaka miegemeo yao. Mawakili wa Gachagua wakishikilia kuwa majaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Freda Mugambi wajiondoe kwenye kesi wakidai hawatatoa haki kutokana na uhusiano wao wa karibu na rais William Ruto, Spika wa Seneti Amason Kingi na naibu rais aliyependekezwa Kithure Kindiki. kadhalika majaji hao wanatoa uamuzi kuhusu agizo la kusitisha kuapishwa kwa kindiki.