Majeshi ya Israeli yaliondoka kutoka katika mji wa Palestina wa Jenin Ijumaa (Septemba 6), wakiacha athari za uharibifu mkubwa wa majumba na miundombinu, kufuatia moja ya operesheni kubwa kabisa ya kiusalama katika eneo ambalo limekuwa likikaliwa kwa mabavu huko Ukingo wa Magharibi kwa miezi kadhaa.
Akihojiwa kuhusu madai ya kuwa eneo hilo lina maghaidi, Samaher Abu Nassa, mkaazi wa eneo hilo la Jenin alisema: Hapana, sisi siyo magaidi, sisi ni watu wa amani. Wao ndiyo magaidi, wanawauwa watoto wetu.”
Jeshi la Israeli lilisema operesheni hiyo ililenga kuzuia vikundi vya wanamgambo vinavyoungwa mkono na Iran kupanga mashambulizi dhidi ya raia wa Israeli.
Limesema kuwa majeshi ya Israeli yamewauwa wanamgambo 14 wakati wa operesheni hiyo, ikiwemo makamanda wa eneo wa Hamas huko Jenin.
Siku ya Ijumaa, maelfu walijiunga katika maziko kuwapeleka makaburini wale waliouwawa wakati wa mapigano.
Wakati majeshi ya Israeli yalijikita hasa katika sehemu kubwa ya mwaka uliopita huko Gaza, Ukingo wa Magharibi umeshuhudia kuongezeka ghasia.
Zaidi ya Wapalestina 680 wameuwawa huko Ukingo wa Magharibi na East Jerusalem, kulingana na wizara ya afya ya Palestina.
#voaswahili #afrika #hezbollah #israel #hamas #fatah #iran #islamicjihad #watoto #vifo #jenin #gaza