Makamu wa Rais JD Vance ahudhuria mkutano wa AI Ufaransa

  • | VOA Swahili
    854 views
    Viongozi wakuu wa dunia wanakutana kujadili masuala ya AI mjini Paris ambako mazungumzo ya kidiplomasia yenye changamoto yanatarajiwa wakati ambapo makundi ya teknolojia yanapigania utawala katika sekta ya teknolojia inayosonga kwa kasi. ⁣ Wakuu wa nchi, viongozi wa juu wa serikali, wakurugenzi wakuu na wanasayansi kutoka nchi 100 wanashiriki katika mkutano wa kimataifa wa siku mbili unaoanza leo Jumatatu.⁣ Wahudhuriaji wakuu ni pamoja na Makamu Rais wa Marekani JD Vance, katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie madarakani, na Makamu wa Waziri Mkuu wa China, Zhang Guoqing. ⁣ Tunaishi katika mapinduzi ya teknolojia na kisayansi ambayo hatujawahi kuyaona, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumapili katika televisheni ya taifa ya Ufaransa. Ufaransa na Ulaya lazima zichukue fursa kwa sababu AI itatuwezesha kuishi vizuri, kujifunza vizuri, kufanya kazi vizuri,⁣ kujihudumia vizuri, na ni juu yetu kuiweka akili mnemba katika utoaji huduma ya binadamu, alisema.⁣ - VOA. ⁣ ⁣ ⁣ ⁣ #akilimnemba #ai #ufaransa #mkutano #teknolojia #makamurais #marekani #jdvance #voa #voaswahili