Mama ambaye hali yake ya kiafya iliangaziwa na KBC apata afueni

  • | KBC Video
    138 views

    Keziah Nyambura ambaye hali yake ya kiafya iliangaziwa na runinga ya KBC CHANNEL ONE hatimaye amepata usaidizi wa kifedha ambao umemwezesha kulazwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu. Kulingana na Nyambura, daktari aliyemhudumia alidokeza kuwa hali yake ilikuwa mbaya na alihitaji uangalizi wa haraka wa matibabu ili kuondoa maji kwenye tumbo lake kabla ya kuendelea na matibabu zaidi. Nyambura alipata usaidizi mwingi wa kifedha kutoka kwa watazamaji wetu uliomwezesha kutafuta matibabu. Mwanahabari wetu, Marie Yambo, anatuarifu zaidi kutoka Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive