Mamia ya wakenya wajitokeza kutafuta kazi za Qatar

  • | Citizen TV
    13,663 views

    Umati wa watu umejitokeza katika jumba la KICC kufuatia tangazo la 𝐃kt. 𝐀𝐥𝐟𝐫𝐞𝐝 𝐌𝐮𝐭𝐮𝐚, kuwa kampuni moja ya Qatari inafanya mahojiano ya kazi humu nchini. kampuni hiyo imetangaza kandarasi za miaka miwili kwa wakenya watakaofaulu kwenye mahojiano. kazi hizo ni za sekta mbalimbali kama vile kwenye mikahawa, madereva, ufundi, ujenzi, na zinginezo. mahojiano hayo yatafanyika kuanzia leo ijumaa hadi jumapili. Willy Lusige anafuatilia matukio hayo na anaungana nasi mubashara kwa mengi zaidi.