Maoni tofauti yaibuka miongoni mwa wakenya kufuatia mkataba wa Rais Ruto na Raila

  • | K24 Video
    46 views

    Siku moja tu baada ya rais William Ruto na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kusaini makubaliano ya kushirikiana, katika juhudi za kupiga jeki maendeleo katika taifa la Kenya .Maoni tofauti yameibuka miongoni mwa idadi kubwa ya wakenya ikiwemo viongozi, baadhi wanamiminia sifa ndoa hii wakidai ni njia ya kuleta umoja nchini , lakini wengine wanaiona kama njama ya kisiasa isiyojali maslahi ya wananchi.