Marekani kushirikiana na Tanzania katika teknolojia ya mtandao

  • | BBC Swahili
    1,927 views
    Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ipo tayari kufanya majadiliano na Marekani kuhusu suala la Visa ya muda mrefu ili kuwawezesha raia wa nchi hizo mbili kunufaika na mpango wa Visa ya muda mrefu. - Kwa upande wake makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amemhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Marekani itashirikiana na Tanzania katika maendeleo ya teknolojia ya intaneti yenye kasi zaidi ya 5G ikiwa ni moja ya kujenga ushirikiano kati ya nchi ya Marekani na Tanzania. Kamala Harris ambaye yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi. 🎥: @mtenganicholaus & @frankmavura #bbcswahili #tanzania #marekani