Marekani na ulimwengu wamepoteza kiongozi wa kipekee marehemu Jimmy Carter- Biden

  • | VOA Swahili
    568 views
    Rais Joe Biden alivunja ukimya akiwa mapumzikoni na familia yake huko Visiwa vya Virgin Islands nchini Marekanikumkumbuka Jimmy Carter, akikumbuka mtangulizi wake kama ni kiigizo kwake na rafiki. Marekani na dunia imepoteza “kiongozi wa kipekee” kufuatia kifo cha Carter, Biden alisema, akiongeza kuwa alikuwa ameongea na watoto kadhaa wa rais huyo wa zamani na alikuwa akishirikiana nao kuandaa rasmi kumbukumbu yake mjini Washington. Akizungumza kwa kiasi cha dakika 10, Biden alimkumbukaCarter kama muungwana na baba wa taifa, mtu ambaye hawezikufikiria aliweza kumpita mtu mwenye shida bila ya kujaribukuwasaidia. “Alisukuma mbele amani, aliendeleza haki za raia, haki zabinadamu, alishawishi uchaguzi huru na wa haki koteulimwenguni,” alisema Biden. "Rais wa Marekani alirejea kumpongeza Carter kwa “tabia zake”na maadili yake, akisema “tabia zilizonjema zimewanyanyua nakubadilisha maisha ya watu mbalimbali na kuokoa maisha yawatu kote ulimwenguni. Biden alisema kuwa ilikuwa “siku ya huzuni” na mojailiyorejesha tena kumbukumbu nzuri za ajabu. Alimkumbuka rais huyo wa zamani wakati akimliwaza yeye namkewe Jill wakati mtoto wao Beau alipofariki kwa saratani mwaka 2015. Rais huyo alisema vile saratani ilivyowaunganisha kati ya familiazao, wakati Carter mwenyewe alipougua saratani katika uhaiwake baadaye. Rais huyo wa zamani wa Marekani Jimmy Carter alifariki akiwa na umri wa miaka 100, baada ya takriban miezi 22 akiuguzwakatika kituo cha hospice kabla ya kufariki. Kituo cha Carter Center kilisema rais wa 39 alifariki Jumapilimchana katika makazi yake huko Plains, Georgia, ambapo yeye na mkewe, Rosalynn, ambaye alifariki Novemba 2023, waliishimuda mrefu zaidi huko. Kituo hicho kilisema alifariki kwaamani, akiwa amezungukwa na familia yake. - AP #JimmyCarter #raiswamarekani #cartercenter #Marekani #maziko #joebiden #rais #marehemu #voa #voaswahili