Margaret Nyakang’o alalamikia uhaba wa fedha unaoendela kuathiri utendakazi wa afisi yake

  • | K24 Video
    80 views

    Mdhibiti wa bajeti Margaret Nyakang’o amelalamikia uhaba wa fedha unaoendela kuathiri utendakazi wa afisi yake. akifika mbele ya kamati ya seneti kuhusu fedha, Nyakang'o alidai kuwa mara kwa mara afisi yake imepokea chini ya asilimia hamsini za fedha wanazohitaji kutekeleza majukumu yake. Nyakang'o amedokeza kuwa ingawa aliomba shilingi bilioni moja nukta sita, afisi yake ilipokea shilingi milioni 777.