Martha Karua adai genge linaloteka nyara wakenya linaamuriwa na rais William Ruto

  • | Citizen TV
    11,654 views

    Kinara wa chama cha Nark - Kenya Martha Karua amedai kuwa Genge linaloteka nyara Wakenya linaamuriwa na rais William Ruto. Katika mahojiano ya moja kwa moja na runinga ya Citizen, Karua amesema kwamba kuna ushahidi kuwa kundi hilo linajumuisha raia wa Kigeni na Wakenya kutoka idara ya Jeshi. Wakati huo huo, Inspekta Generali wa Polisi Douglas Kanja amesisitiza kwamba wanaotekeleza uhalifu huo sio maafisa wa Polisi.