Mashabiki wa Taifa Stars wakihamasisha timu yao kufuzu kuingia AFCON 2025

  • | VOA Swahili
    947 views
    Mashabiki wa Tanzania -Taifa Stars wakishangilia timu yao katika mchezo wa kufuzu kuingia kwenye michuano ya Afcon 2025 kati ya timu ya Taifa Stars (Tanznaia) na DRC- Lepoard kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa mjini Dar es Salaam ambapo DRC waliibuka na ushindi wa bao 2-0. Taifa Stars imepoteza mchezo wa marejeano wa kufuzu fainali za AFCON 2025 dhidi ya DR Congo kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mabao ya Congo yamefungwa na mshambuliaji Meshack Elia katika dakika za 88 na 90+, nyota huyo akiitumikia Young Boys ya Uswisi katika ngazi ya klabu. Hadi sasa kwenye msimamo wa kundi H, linaongozwa na DR Congo wenye pointi 12 ambao tayari wamefuzu kwenye fainali hizo, Tanzania (Taifa Stars) nafasi ya pili ikiwa na pointi 4, Guinea nafasi ya tatu pointi 3, Ethiopia ikishika mkia ikiwa na pointi 1. #tanzania #afcon2025 #drc #naibuwaziri #hamismwinjuma #daressalaam #benjaminmkapa #uwanja