Mashindano ya wanaskauti Nyanza yamekamilika huko Nyamira

  • | Citizen TV
    185 views

    Huku mashindano ya wanaskauti kutoka ukanda wa Nyanza yakikamilika katika shule ya upili ya wavulana ya Nyansiongo kaunti ya Nyamira, Wakenya wamehimizwa kujitahidi zaidi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mashindano hayo yaliyowashirikisha wanaskauti zaidi ya 4,500 kutoka shule 256 yanalenga kuwafundisha vijana maadili mema, mbinu za kujikimu kimaisha, na mbinu mwafaka za kutunza mazingira. viongozi wa muungano huo wamewahimiza wanafunzi, wazazi na walimu kujiunga na muungano huo unaolenga kukuza maadili mema.