Mashirika ya HAART na Polisi Aid yawasaidia waathiriwa ulanguzi wa binadamu

  • | KBC Video
    49 views

    Shirika lisilo la kiserikali linalotoa hamasisho dhidi ya ulanguzi wa binadamu lenye makao yake jijini Nairobi kwa ushirikiano na shirika la Polish Aid, limezindua mradi wa kuwapa waathiriwa ujuzi muhimu wa kibiashara na usaidizi wa kiuchumi Hadi kufikia sasa, waathiriwa 60 wamepokea msaada kutoka kwa mashirika hayo mawili kupitia ubalozi kwa Jamhuri ya Poland humu nchini. Msaada huo ni sehemu ya mpango makhsusi ulioanzishwa mnamo mwaka wa 2010 ambao unanuiwa kutambua na kusaidia zaidi ya waathiriwa 1000 wa ulanguzi wa binadamu. Wanaonufaika wanatumia misaada hiyo pamoja na ujuzi kufanikisha maisha yao na kuchangia ukuaji wa kiuchumi pamoja na kuzisaidia jamii zao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive