Mashirika ya haki kutoka Mombasa yakosoa utekaji nyara nchini

  • | Citizen TV
    2,801 views

    Wakati huo huo, mashirika ya kutetea haki kutoka maeneo ya Pwani pia yamemtaka Inspekta wa polisi Douglas Kanja kujiuzulu kwa kile wanachodai ameshindwa kudhibiti visa vya utekaji nyara nchini. Wakiongea katika eneo la Likono kaunti ya Mombasa, mashirika hayo yamesema ni kinaya kuwa polisi wamejitenga kuhusika ilhali ni jukumu lao kuhakikisha usalama wa wakenya.