Mashirika ya kijamii yatoa wito kwa polisi kuwalinda watu walio na ulemavu

  • | KBC Video
    8 views

    Baadhi ya mashirika ya kijamii kaunti ya Nairobi yametoa wito kwa idara ya polisi kuwalinda watu walio na ulemavu dhidi ya dhulma za kijinsia.Wakizungumza baada ya matembezi ya kuadhimisha kampeni ya siku 16 za kupambana na dhulma za kijinsia, viongozi wa mashirika hayo walisema kwamba mara nyingi watu walio na ulemavu hawapati haki baada ya kudhulumiwa kijinsia kutokana na hali yao. Hata hivyo maafisa wa polisi waliojitokeza kwenye matembezi hayo waliwahakikishia usalama wa kutosha na kuhimiza jamii hiyo kujitokeza kudai haki wanapodhulumiwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive