Masomo katika shule 14 zilizoko Baringo yarejea baada ya amani kuanza kushuhudiwa

  • | Citizen TV
    383 views

    Masomo katika shule kumi na nne zilizoko kaskazini mwa bonde la ufa yameanza kurejelewa baada ya amani kuanza kushuhudiwa katika maeneo yaliyokabiliwa na utovu wa usalama. shule hizo zilikuwa zimefungwa kwa miaka mitatu kutokana na ukosefu wa usalama na uvamizi wa majangili. Na kama anavyoarifu Brenda Wanga,maafisa watano wanashika doria katika kila shule ili kuhakikisha masomo yanaendelea.