Maswali yaibuka kuhusu shahada ya heshima aliyopewa mbunge Oscar Sudi

  • | Citizen TV
    60 views

    Shahada ya heshima maarufu kwa kiiengereza honorary degree iliyopewa wabunge Oscar Sudi, Didmus Barasa na John Waluke imezua mijadala na kuvutia shutuma kutoka kwa taasisi za mbali mbali ikiwemo taasisi ya wahandisi humu nchini. Kulingana na taasisi hiyo, baadhi ya shahada na mataji ambayo hukabidhiwa wasomi hutokana na muda mrefu wa kusoma na mafanikio katika masomo ya juu. Na sasa tasisi ya wahandisi inasema imekerwa na hatua ya mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi ya kutumia taji la mhandisi licha ya kuwa na uzoefu huo. Je, utoaji wa shahada za heshima umepita umekosa uadilifu?