Matembezi ya uhisani : Miradi mbalimbali ya kijamii kufadhiliwa

  • | KBC Video
    1 views

    Zaidi ya watu 200 walishiriki katika makala ya kwanza ya matembezi ya uhisani ALMAARUFU March in March katika mtaa wa Karen kaunti ya Nairobi. Washiriki hao wengi wao wanawake walitembea umbali wa kilomota-5.5 na kilomita-4.7 kutoka barabara ya Kombe hadi bustani ya Karen Waterfront. Mtembezi hayo yaliandaliwa na wakfu wa Intrepid kwa lengo la kukusanya fedha za kufadhili mipango ya kukabiliana na uwindaji haramu wa wanyamapori katika hifadhi ya Mara, kuwawezesha wanawake wa jamii ya Wa-masaai kubuni nafasi za ajira, kutoa baiskeli kwa watoto waoenda shuleni katika maeneo ya mashambani na wahudumu wa afya humu Kenya. Matembezi hayo yataandaliwa kila mwaka huku kukiwa na uwezekano kushirikisha riadha ili kuwavutia washiriki zaidi ambao wangependa kushiriki katika mbio.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive