Matibabu ya ukimwi, Kifua kikuu na Malaria kuathiriwa kufuatia agizo la Trump

  • | KBC Video
    152 views

    Serikali inaweka mikakati ya kukidhia nakisi iliyotokea kufuatia hatua ya Marekani ya kusitisha ufadhili wa shirika la USAID ambalo lilikuwa linafadhili baadhi ya huduma za afya humu nchini. Kulingana na waziri wa afya Dkt. Deborah Barasa, taifa hili linajitahidi kujumuisha ushughulikiaji maradhi ya UKIMWI na kifuakikuu katika mfumo wa huduma za matibabu hapa nchini. Kulingana na Barasa, halmashauri ya afya ya jamii-SHA itakuwa muhimu katika kuhakikisha huduma za matibabu ya virusi vya HIV na TB zinaendelea kutolewa kufuatia kusitishwa kwa ufadhili wa kigeni. Shirika la USAID tayari limetangaza kwamba litawapeleka wafanyikazi wake wote kote ulimwenguni kwa likizo kuanzia Ijumaa ijayo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive