Mauaji ya Gen Z: Mashirika ya haki yataka polisi kuwajibishwa

  • | Citizen TV
    487 views

    Mashirika ya haki nchini sasa yanataka mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuweka bayana orodha ya watu walioshtakiwa kuhusiana na mauaji ya vijana wakati wa maandamano ya Gen Z mwaka jana. Shirika la Amnesty International likirejelea ripoti ya punde zaidi ya upekuzi wa shirika la habari la BBC ulioonyesha wazi maafisa waliohusishwa na mauaji ya vijana hao.