Mbappe ajiunga na Real Madrid

  • | VOA Swahili
    589 views
    Kylian Mbappe hatimaye amevaa jezi ya timu ya Real Madrid kutimiza ndoto yake ya utotoni katika uwanja uliofurika wa Santiago Bernabeu. Takriban mashabiki 80,000 walijitokeza katika uwanja wa Bernabeu kumkaribisha nyota wa Ufaransa wakati wa kujitambulisha rasmi kama mchezaji mpya kabisa wa klabu hiyo. Alisaini rasmi mkataba wake wa miaka mitano na timu hiyo maarufu ya Uhispania akiwa na rais wa klabu hiyo Florentino Perez na baadaye akajitokeza katika jukwaa kuwasalimia mashabiki wa Madrid. - AP #football #mbappe #realmadrid #voa