Mfanyabiashara aomba serikali iwawekee kodi moja

  • | VOA Swahili
    429 views
    Video hii imechukuliwa katika soko la Kituku liliyopo kwenye bandari ndogo ambayo inapokea wafanyabiashara wengi na wakulima kutoka kwenye vijiji mbali mbali huko Kivu Kaskazini na Kivu Kusini. Kati yao ni wafanyabiashara wa mkaa na watu wanao fika bandarini kwa kutumia boti wakitoka vijijini na wengine wakiondoka kwenda vijijini ambako wanafuata mazao ya chakula, boti zote wanazotumia zimetengenezwa kwa mbao. Boti hizi hubeba mkaa, ndizi, mbuzi na vitu vingine kuja Goma ambako kuna maelfu ya watu wanaopitia hali ngumu ya kimaisha. Sehemu hii kuna soko. Vile vile kuna shughuli za usafirishaji, ndiyo sababu utawakuta watu wengi wapikipiki wakisubiri wateja na kuwapeleka katikati ya Mji ambako sasa biashara mbalimbali huuzwa barabarani ama kwenye baadhi ya maduka. Watumiaji wa piki wakilalamikia hali ya Maisha kuwa ngumu kutokana na vita mashariki mwa Congo hasa hivi vya M23 ambavyo vimeathiri shughuli zote Mjini Goma na Kote Kivu kaskazini kutokana na vijiji vingi kuchukuliwa na waasi hao na kupelekea wakulima kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi katika mji wa Goma. Sikiliza pia malalamiko ya kodi zinazotozwa ambazo zimekuwa kero kwa wananchi. Endelea kusikilzia mfanyabiashara aliyehojiwa na mwandishi wetu Austere Malivika huko mji wa Kituku akieleza... #goma #kivukaskazini #jimbo #waasi #m23 #raia #makombora #sake #gavana #cirimwani #mejajenerali #voa #voaswahili