Mgombeaji uenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika, Raila awaambia vijana wawe na imani na serikali

  • | K24 Video
    111 views

    Mgombeaji uenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika, Raila Odinga amewaambia vijana wawe na imani na serikali wakati huu ambao taifa linapitia changamoto za kijamii na za kiuchumi. Raila amewataka vijana wajitenge na msukumo wa kusababisha msukosuko na kuwa sehemu ya upatikanaji wa suluhu nchini. Raila alikuwa akizungumza wakati wa hafla ya kufuzu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Kabarak.