Migori yaanzisha mfumo wa kidijitali wa kukusanya mapato

  • | Citizen TV
    76 views

    Uzinduzi wa mfumo wa kidijitali wa kukusanya mapato katika kaunti ya Migori unalenga kuimarisha ufanisi na kuziba mianya ya wizi wa fedha za umma zinazokusanyw ana kaunti hiyo. Mfumo huo ambao utatumiwa kwenye huduma zote za kaunti hiyo unakisiwa kuwa utaleta uwazi na kuhakikisha uwajibikaji wa maafisa wa kaunti , kando na kurahisisha ukaguzi wa rekodi za walipa ushuru. Kulingana na Mkurugenzi wa mapato wa kaunti Maurice Oindo, mfumo huo mpya utafuatilia vyanzo vyote vya mapato ikiwa ni pamoja na ada za soko, kodi, ada za maegesho na leseni za biashara kwa urahisi. Migori inalenga kukusanya shilingi bilioni moja mwaka ujao wa kifedha.