Mirindimo ya kisiasa yazidi kutolewa Mlima Kenya

  • | KBC Video
    96 views

    Mchecheto wa kisiasa katika ukanda wa Mlima Kenya umeendelea kushika kasi huku baadhi ya viongozi kutoka eneo hilo wakionekana kutoa hisia zao kuhusu hali ilivyo nchini. katika hafla ya leo ya mazishi ya nduguye gavana wa Meru Kawira Mwangaza, Eric Kimathi, almaarufu steero iliyofanyika katika eneo la Mathagiro eneo bunge la Buuri Kaunti ya Meru, gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga alimtaka gavana wa Tharaka Nithi aliyekuwepo katika mazishi hayo, kumrai naibu wa rais Kithure Kindiki kuzuru kaunti yake ya nyumbani ya Tharaka Nithi.Kwa upande wake,gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki alimtaka kahiga kumkumbatia na kumkubali Kindiki kama naibu wa rais.Aidha viongozi hao wameitaka serikali kutimiza ahadi ilitoa kwa wananchi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive