Miti iliyopandwa na waasisi wa Umoja wa Afrika miaka 62 iliyopita

  • | VOA Swahili
    208 views
    Umoja wa Muungano wa Afrika (OAU), ambayo hivi sasa ni Umoja wa Afrika (AU), uliundwa Mei 25, 1963, huko Addis Ababa, Ethiopia, kukuza umoja na mshikamano kati ya nchi za Afrika na kuchangia katika maendeleo ya uchumi, kijamii na kisiasa barani humo. OAU iliasisiwa na mataifa ya Kiafrika 32 ambayo yalikuwa yamejipatia uhuru. Tukio la kukumbukwa wakati umoja huo unaundwa ilikuwa ni upandaji mti uliofanywa na viongozi wa mataifa hayo 32. Miaka 62 baadaye, miti hiyo bado inaendelea kuwa ni kivutio kinachoonekana huko Addis Ababa, ambapo watu huketi katika vivuli vya miti hiyo. Katika Mkutano wa 38 wa AU, mwandishi wa VOA Kennedy Abate alitembelea eneo la Afrika Park kuchukua picha za miti hiyo iliyopandwa na Mfalme Haile Selassie, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, na viongozi wengine waasisi. #AU #africanunion #ethiopia #voa