Mjasiriamali aeleza changamoto za biashara ya unoaji visu

  • | VOA Swahili
    257 views
    Salum Ally ni Mkazi wa Dar es Salaam alieamua kujiajiri kupitia unoaji wa visu na mapanga majumbani. Hivi sasa kazi hiyo imekuwa chanzo kikuu cha mapato kwake yeye na familia yake ambapo kazi hiyo inampa fursa ya kusomesha watoto wake pamoja na kukidhi mahitaji ya familia yake licha ya changamoto anazokutana nazo. Kwa upande wa wateja wa biashara hiyo ya unoaji visu wameeleza namna gani wananufaika na kazi ya unoaji majumbani inayofanywa na Ally wakisema kazi hiyo inawarahisishia kupata huduma ya kunolewa visu vyao majumbani bila kufika katika maeneo ya masoko ambapo ndipo wanoaji hupatikana kwa wingi anaeleza Sheyma Ayoub, Mkazi wa Dar es Salaam. #visu #unaoaji #salumally #mkazi #daressalaam #familia #mjasiriamali #biashara #voaswahili #voa