Mjasiriamali atoa ushauri kwa vijana kuchangamkia fursa

  • | VOA Swahili
    151 views
    Mzee Zubery Shamte, mfanyabiashara wa kuchinja na kunyonyoa kuku kutoka Njia ya Ng’ombe, Mbagala, awahamasisha vijana kushikamana na kazi kwa bidii licha ya changamoto zinazojitokeza. Ameeleza kuwa biashara ina changamoto zake, kama vile ukosefu wa wateja kwa muda mrefu, lakini uvumilivu, imani, na maamuzi sahihi vimekuwa nyenzo muhimu katika mafanikio. Amewashauri vijana kuchangamkia fursa kwa juhudi na kutumia akili, na amesisitiza kuwa nia thabiti na maadili mema vinaweza kusaidia kuvuka changamoto na kufanikisha maisha. Ripoti ya mwandishi wa VOA Amri Ramadhani, Dar es Salaam, Tanzania #mjasiriamali #mbagala #daressalaam #tanzania #kuku #kazi #vijana #fursa #uvumilivu #imani #maamuzi #voa #voaswahili