Mkazi wa Gaza asema Wapalestina wanaimani na mahakama ya UN

  • | VOA Swahili
    917 views
    Wapalestina huko Rafah waitaka mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa kusimamisha kabisa vita vya Israel na Hamas, kuwapa haki yao Wapalestina, na kuamrisha malipo ya juhudi za ujenzi mpya huko Gaza. Majaji kwenye mahakama ya Kimataifa ya Haki Alhamisi wameanza siku mbili za kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini, ikiishutumu Israel kwa kutekeleza mauaji ya kimbari katika vita vyake huko Gaza. Afrika Kusini imeiomba mahakama hiyo iamuru kusitishwa mara moja kwa kampeni ya Israel huko Gaza, ambako Israel imesema kwamba nia yake ni kuliangamiza kundi la Hamas, kufuatia shambulizi la Oktoba 7 kusini mwa Israel. Wesam Dardouna kutoka eneo la Jabaliya akitoa hisia zake kuhusu kesi hiyo anaeleza: “Matumaini yetu kuwa mahakama hii ya kimataifa itasimamia haki za Wapaletina wote. Tunamatumaini makubwa na mahakama hii kwamba italaani kile Israel ilichofanya, Kwa sababu imetekeleza mauaji makubwa na ya kimbari dhidi ya kaskazini (mwa Gaza) na katikati ya Gaza na dhidi ya watu wote. Aliongeza kusema: Kunauharibifu katika kila nyumba na pia waliokufa mashahidi 'katika kila nyumba na waliojeruhiwa.” Shambulizi lililofanywa na Hamas Oktoba 7 kwa kuvuka Gaza na kuingia kusini mwa Israel lilisababisha vita na waliwauwa kiasi cha watu 1,200.⁣ Mashambulizi ya Israel ya angani, ardhini na baharini huko Gaza yameuwa zaidi ya Watu 23,000, theluthi mbili kati ya hao ni wanawake na watoto, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo la Gaza linalosimamiwa na Hamas.⁣ Idadi hiyo haitofautishi kati ya raia na wanamgambo. - AP ⁣ #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #westernwall #mateka #jeshi #mahakama #umojawamataifa #mauaji #kimbari