Mkulima Makueni akumbatia kilimo asilia

  • | KBC Video
    42 views

    Mkulima mmoja katika kaunti ya Makueni amekumbatia kilimo asilia huku akitumia sayansi ya kisasa kuimarisha uzalishaji chakula na kuzuia kuangamia kwa aina fulani za mimea na wanyama. Benedetta Kyengo amehamia kilimo hicho wakati ambapo afisi ya umoja wa mataifa ya kukabiliana na majanga inakadiria kwamba angalau asilimia-30 ya viumbe hai wanaangamia kutokana na matumizi mabaya ya udongo. Kutoweka kwa viumbe hai kunasababisha uwepo wa gesi inayojulikana kama ‘laughing gas’ inayoharibu utandu wa ozoni na kuongeza kiwango cha mionzi hatari ya jua duniani. Mwanahabari wetu Opicho Chemtai alizuru shamba la mkulima huyo na kutufafanulia kwamba uwpo wa gesi ya ‘laughing gas’ sio jambo la mzaha.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive