Mmiliki wa kiwanda cha gesi kilichosababisha moto Nairobi ajisalimisha polisi

  • | VOA Swahili
    47 views
    Hatimaye mmiliki wa kiwanda cha gesi kilicholipuka eneo la Embakasi, jijini Nairobi amejisalimisha kwa polisi na kukana mashtaka yanayomkabili. Wataalam wa mipango ya miji nchini Kenya wanazidi kushangazwa kuwepo kiwanda hicho katika eneo wanapoishi wakazi, wakati huo huo familia nyingi zimeachwa bila makao, huku watu sita wakipoteza maisha yao. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.