Mpango wa Barabara Kuu Utaunganisha nchi 5 Afrika

  • | VOA Swahili
    88 views
    Nchi za Afrika Magharibi zinashinikiza kujengwa kwa mtandao wa barabara kuu zinazounganisha nchi tano kutoka Ivory Coast hadi Nigeria. Benki ya Maendeleo ya Afrika inasema mradi huo utakuwa ni kichocheo cha uchumi kwa nchi zote husika. Senanu Tord anaripoti kutoka Accra, Ghana. Nii Annan Ofori ni kiongozi wa kijadi na msimamizi wa ardhi katika eneo la kitamaduni la Ga East nje kidogo ya mji mkuu wa Ghana, Accra. Jamii yake imechaguliwa kunufaika na sehemu ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1028 inayoanzia Abidjan hadi Lagos. Barabara ya chini ya ardhi yenye urefu wa kilomita tatu itapita katika eneo la jamii hii. Mpango huu unaangazia siku za usoni kuiunganisha barabara hii na nchi nyingine, ili kuwa na mtandao mpana katika bara hilo lenye barabara kuu 9 zinazoanzia Cairo hadi Cape Town na kutoka Dakar hadi Djibouti. Hatua ijayo, kulingana na Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ni kuiunganisha Dakar hadi eneo la Abidjan na Lagos. - VOA Senanu Tord, VOA News, Accra Ghana #SenanuTord, #VOANews, #Accra #Ghana #afrikamagharibi #ADB #niiannanofori #kiongozi #jadi