Msaidizi wa kibinafsi wa Gavana Sakaja atekwa nyara

  • | KBC Video
    160 views

    Mahakama kuu imeagiza uchunguzi uharakishwe katika kisa cha kutekwa nyara kwa Osman Khalif ambaye ni msaidizi wa kibinafsi wa gavana wa Nairobi Johnson Sakaja aliyetoweka hivi majuzi. Jaji Chacha Mwita ameagiza polisi kuchukua hatua haraka na kuwakamata wanaodaiwa wamteka nyara. Aidha, jaji huyo pia alimwagiza mshirikishi wa upelelezi wa jinai katika eneo la Nairobi Peter Njeru pamoja na polisi kutumia teknolojia ikiwemo camera za CCTV zilizoko kituo cha Sarit Centre kukusanya ushahidi na taarifa zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa watekaji nyara hao. Maelezo zaidi ni kwenye makala ya mizani ya haki.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News