Msambweni One yaanza kinyang’anyiro cha Dola Super Cup kwa ushindi wa 2-1

  • | Citizen TV
    112 views

    Msambweni One Fc walifungua kampeni yao ya mchuano wa Dola Super Cup awamu ya Kwale kwa kuilaza Lungalunga one kwa mabao mawili kwa moja. Kwenye mechi hiyo ya ufunguzi iliyochezwa uwanjani ukunda show kaunti ya kwale, Msambweni ilitumia vyema fursa ya kucheza mbele ya mashabiki wake na kushinda mechi hiyo muhimu. Mshindi wa mashindano hayo yanayochezwa ndani ya ukanda wote wa pwani atazawadiwa shilingi milioni moja miongoni mwa zawadi nyingine.