MSF yasema hali ni mbaya Ituri, mashariki mwa DRC, katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    10,736 views
    Shirika la misaada ya kibinadamu la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limeonya kwamba hali katika jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inazidi kuwa mbaya. MSF inasema watu huko wanakabiliwa na mashambulizi ya vurugu, kulazimishwa kukimbia nyumba zao, na kuhangaika kupata huduma za matibabu. Katika ripoti hiyo mpya, MSF inasema maisha yanazidi kuwa hatari zaidi kwa jamii zilizoko kwenye mzozo huko mashariki mwa DRC, ambapo Umoja wa Mataifa unasema mapigano hayo yamewafanya zaidi ya watu laki moja kukosa makazi. Tangu mwanzo wa mwaka huu, zaidi ya watu 200 wameuawa katika mashambulizi, na wengine wengi kujeruhiwa. MSF inasema madaktari wao wamewatibu manusura wa mashambulizi ya mapanga na risasi, wakiwemo watoto na wanawake wajawazito.