Mvutano kati ya kaunti ya Nairobi na kampuni ya umeme KPLC

  • | Citizen TV
    2,947 views

    Mzozo umeibuka kati ya serikali ya kaunti ya Nairobi na kampuni ya kusambaza umeme ya Kenya Power baada ya maafisa wa kaunti kumwaga taka nje ya makao makuu ya kampuni hiyo mtaani Ngara, Nairobi. Hatua ya serikali ya kaunti ilifuatia uamuzi wa Kenya Power kukatiza huduma za umeme wiki iliyopita wakidai malipo. hata hivyo umeme ulirudishwa baada ya serikali ya kaunti kutoa ahadi ya kulipa shilingi milioni 133 za kupunguza deni hilo. .