Mwaka mpya wa 2025 wakaribishwa kwa mbwembwe kote duniani

  • | KBC Video
    145 views

    Maeneo ya burudani jijini Nairobi yalifurika mkesha wa mwaka mpya, huku wateja wakimiminika maeneo hayo ili kuukaribisha mwaka mpya wa 2025 kwa mitindo mbali mbali.Biashara ilinoga kwa wamiliki wa vituo hivyo, ambao walisema mwaka 2024 ulikuwa mgumu kutokana na nyakati ngumu za kiuchumi zilizosababishwa na gharama ya juu ya maisha. Hata hivyo walielezea matumaini yao kwamba mwaka 2025 utakuwa wenye ufanisi. Katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta KICC, wakenya walijitokeza kwa idadi kubwa kushuhudia maonesho ya kufana ya fataki. Ripota wetu Timothy Kipnusu anatupa taswira ya jinsi wakenya walivyoukaribisha mwaka mpya wa 2025.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive